Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 21, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA VIWANJA VYA AZAM LEO, AZIPONDA SIMBA NA YANGA


Rais  Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Uwanja wa Azam uliopo Mbande, Temeke Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Bakharessa, Abubakar Bakharessa na  wa kwanza kushoto ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,  Dk. Fenella Mukangara na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Mecky Sadick. 

Rais akipokea zawadi ya jezi toka kwa Abubakar Bhakherssa ambaye ni mkurugenzi wa wakurugenzi wa kampuni ya Bakharessa

Rais akisogeza kitambaa kuashiria uzinduzi 

Hapa anatembezwa kwenye uwanja wa nyasi bandia

Hapa anatembezwa uwanja wa nyasi asilia

Rais akisalimia na wachezaji wa Azam A kabla ya kuanza mchezo ndidi ya Azam B

Makocha wa Timu za Taifa na viongozi mbalimbali wa TFF walikuwepo

Hapa yupo kwenye swimming pool 

Burudani pia ilikuwa sehemu ya sherehe

"Lazima mtuchangie vijana wenu" Wacheza ngoma wakitembeza bakuli baada ya kucheza bila kuona mtu aliyekuja kuwatunza

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr.Jakaya Kikwete leo amezindua rasmi uwanja wa Azam na kuziponda Simba na Yanga kwa kushindwa kumiliki viwanja vyao wenyewe badala yake wameendeleza migogoro

Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Dar es Salaam alipata wasaa wa kuzungumza na maelfu ya wakazi wa jiji hili baada ya kujionea kazi nzuri inayofanywa na Azam na kuipongeza kwa kufanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano ya shirikisho.


"Naipongeza Azam kwa kuwekeza kwenye ufundi na siyo kamati za ufundi kama zinavyofanya vilabu vyetu vikubwa kwa maana kama ingekuwa kamati za ufundi zinasaidia bara la afarika tungekuwa tunachukuwa kombe la dunia kila linapofanyika" alisema Rais

Wakati akiyasema hayo maelfu ya watu walikuwa wakimshangilia kwa kuonyesha kuwa nachokisema ni kweli.


No comments:

Post a Comment