Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 3, 2013

LIBOLO YATUMIA UWANJA KUIUA SIMBA, ZAIDI FUATILIA HABARI HII

BENCHI la ufundi la Simba SC jana limeukagua Uwanja wa Estadio Libolo itakakochezwa mechi ya  ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya Wekundu na Libolo na kubaini siri nzito.

Vipimo vya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, vilibaini kwamba uwanja huo una upungufu wa takribani mita sita kwa urefu na upana kulinganisha na viwanja vingi vya soka.

Kwa mujibu wa Liewig, uwanja huo umepunguzwa ukubwa ili kusaidia timu ya Libolo ambayo inafahamika sana kwa kufunga mabao mengi ya mipira iliyokufa (adhabu, kurusha n.k).

“Kutokana na hali hii, maana yake ni kwamba kila itakapokuja kona, itakuwa hatari kwa sababu kuna umbali mdogo kutoka kwenye kona hadi goli. Itakuwa hatari hivyohivyo kwenye mipira ya kurusha na ya adhabu. Ni muhimu tumeliona hili mapema,” alisema.

Alisema atawaeleza wachezaji wake kujiepusha kutoa kona au mipira ya kurusha bila ya sababu kwa vile inaonekana hiyo ndiyo silaha kubwa ya wapinzani hao wa Simba.

“Kama unakumbuka, hata goli lao la Dar lilitokana na mpira wa kurusha halafu ikapigwa krosi. Ndiyo maana nafikiri wameleta mechi hii huku badala ya Luanda ili watumie faida hii vizuri,” alisema.

Nchini England, Uwanja wa Britannia unaotumiwa na timu ya Stoke City inayocheza Ligi Kuu ya nchi hiyo unafahamika pia kwa kuwa mdogo kwenye eneo la kuchezea kuliko viwanja vingi vya nchi hiyo.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba lengo kuu la kuuweka uwanja huo katika eneo hilo ni kutumia nguvu ya mipira ya kurusha na adhabu nyingine ambayo ndiyo silaha kubwa ya Stoke. Miaka miwili iliyopita, robô ya magoli yaliyokuwa yakifungwa na timu hiyo yalitokana na mipira ya kurusha ya Rory Delap

No comments:

Post a Comment