Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 24, 2013

HARAMBEE STARS NA SUPER EAGLES NGUVU SAWA

Harambee Stars ya Kenya licha ya kupata mateso tangu wawasili nchini Nigeria kucheza na Super eagles katika mechi ya kutafuta kuingia katika kombe la dunia Jumamosi nusura wawaaibishe mabingwa wa Afrika kwa kutoka sare ya 1-1 huko mjini Calabar , Nigeria. 

Kenya ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia mchezaji Francis Kahata katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza.
Licha ya Sduper Eagles kuwateremsha miamba yake yote kama vile John Obi Mikel na Victor Moses wa Timu ya Chalsea ya Uingereza lakini hawakufua dafu kwa kenya hadi katika dakika za majeruhi ya kipindi cha pili.
Katika dakika hizo za majeruhi mchezaji Nnamdi Oduamadi aliiondolea Super Eagles aibu kwa kufunga bao na punde tu firimbi yamwisho kumaliza mechi ikapulizwa.
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ni katika mechi ya kirafiki mwezi Machi, 2011 Mjini Abuja ambapo Super Eagles ilifunga 3-0. 

 
VIKOSI:
Wachezaji Harambee Stars: Arnold Origi, David Owino, Mulinge Munandi, David Ochieng, Brian Mandela, Victor Wanyama, David Gateri, Johanna Omollo, Jamal Mohammed, Dennis Oliech and Francis Kahata. Coach Adel Amrouche 

Wachezaji wa Super Eagles: Vincent Enyeama, Solomon Kwambe, Godfrey Oboabona, Kenneth Omeruo, Elderson Echejile, Sunday Mba, Mikel Obi, Eddy Onazi, Obafemi Martins, Victor Moses and Brown Ideye 


Waamuzi 
Referee: Joshua BONDO (BOT)
Assistant Referee 1: Meshack MEDUPI (BOT)
Assistant Referee 2: Moemedi MONAKWANE (BOT)
Fourth official: Kutlwano LESO (BOT

No comments:

Post a Comment