Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, January 24, 2013

UKUMBI WA CCM TANDALE KUWAKA MOTO JANUARI 27, KUTAKUWEPO NA NDONGA ZA KUFA MTU

SUPER D BOXING COACH



 
 
 
 
 
 
 
 
Mabondia Hassan Mandulla na James Martin wanatarajia kupanda ulingoni Januari 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandale Dar es salaam.

Akizungumzia mpambano huo mwandaaji Waziri Rosta amesema kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo ya mabondia maarufu na chipukizi alisema mapambano ya utangulizi ni Fadhiri Majia na Anton Matiasi mpambano mwingine

Utawakutanisha Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma na Charles Mashali atavaana na Adam Ngange, Julias Noro atapambana na Abdallah Luwaje mpambano mwingine utawakutanisha Rajabu Tumaini na Daudi Antony na Rashid Mohamed atavaana na Eliman Richard wakati Rashid Hamisi atamvaa Omary Shabani


Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina
michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibu Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.  

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

No comments:

Post a Comment