Shirikisho la soka nchini (TFF)
limewaonya watu walioanza kampeni za kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo kabla tarehe
haijatangazwa.
Kwa mujibu
wa taarifa zilizopo, baadhi ya watu wenye nia ya kugombea tayari
wameanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi huo wakati bado kamati
inayosimamia uchaguzi haijatoa ruhusa.
Uchaguzi huo ambao rais
wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, hawezi kugombea tena kwa mujibu wa
katiba, umepangwa kufanyika mwezi ujao katika sehemu ambayo itatangazwa.
Katibu
wa TFF, Angetile Osiah, amesema ruhusa ya kuanza kwa kampeni za
uchaguzi huo bado haijatolewa na kamati inayosimamia uchaguzi.
Alisema watu wenye nia ya kugombea walioanza kampeni hizo wanakwenda kinyume na taratibu za uchaguzi mkuu.
Osiah
amesema hakuna ruhusa kwa mtu yeyote kuanza kampeni kabla ya tarehe ya
uchaguzi kutangazwa na kwamba anayefanya hivyo anakiuka sheria za
uchaguzi.
Amesema kampeni ni hatua za mwisho za uchaguzi na
zinaruhusiwa kufanyika baada ya kutangazwa na kuongeza huwezi kuanza
kampeni wakati tarehe za uchaguzi na utoaji fomu bado hazijajulikana.
Amesema
kuwa TFF itawachukulia hatua kali watakaobainika kuanza kampeni hizo
huku akisisitiza wasubiri muda sahihi ufike ndiyo waanzae kampeni zao.
TFF
itatoa taarifa kamili kuhusiana na uchaguzi huo zitajulikana kesho
baada ya kamati ya utendaji kumaliza kikao chake na kutoa tamko rasmi la
lini na wapi uchaguzi mkuu utafanyika.
Viongozi wa kuchaguliwa
wa TFF waliopo madarakani tayari wamemaliza muda wao, huku rais Tenga
hatagombea tena mwaka huu, kwa mujibu kamati ya uchaguzi mkuu.
No comments:
Post a Comment