Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, October 8, 2012

PAMBANO LA SIMBA, OLJORO JKT LAINGIZA MIL 46/-

Kikosi cha Simba

Kikosi cha JKT Oljoro

Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT ya Arusha lililochezwa Oktoba 7 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 limeingiza sh. 46,680,000.
 
Watazamaji 8,081 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,172,396.61 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,120,677.97.
 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 193,000, waamuzi sh. 210,000, mwamuzi wa akiba (fourth official) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,175,000. Gharama za mchezo sh. 2,724,132.20, uwanja sh. 2,724,132.20, Kamati ya Ligi sh. 2,724,132.20, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,634,479.32 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,089,652.88.
 

No comments:

Post a Comment