Ngassa akiwa amemiliki mpira huku beki wa Transist Camp akiwa amemkaba vilivyo |
Ashanti United |
Transist Camp |
Wachezaji wa akiba Ashanti |
Wachezaji wa Akiba Transist |
Mdundiko wa Ashanti kama kawaida yao |
Jerome Lambele mfungaji wa mabao yote ya Ashanti leo |
Mwenyekiti wa Chama cha soka manispaa ya Ilala Kasongo akiwapongeza wachezaji baada ya mchezo kumalizika |
TIMU ya Ashanti United ya Ilala imewachezesha kwata timu ya wanajeshi wa Transit Camp mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Ashanti ambao wanaonyesha wanataka kurudi ligi kuu walilishambulia lango la Transist Camp muda wote na kufanikiwa kupata mabao yote kupitia kwa Lambele Jerome dakika za 19, 41, 54 na 89 na Transist Camp walijipatia bao lao kupitia kwa Kombo Kombo dakika ya 31.
Transist Camp walipata pigo baada ya mchezaji Masoud Omari kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 65.
Kocha wa Transist Camp Hajj Othman aliwatupia lawama waamuzi na kusema kuwa alikuwa alikuwa anaipendelea Ashanti.
Naye Jamhuri Kiwelu "Julio" kocha wa Ashanti alisema ndio kwanza wameanza safari na hawategemei kuwa kuna wa kuwasimamisha ila hakuaacha kuwasifia wa chezaji wake kwa kufuata vema mafundisho yake na ndio maana wamefanya vema.
Matokeo mengine kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi Tessema ya Temeke imeifunga Villa United ya Kinondoni bao 1-0 lililofungwa na Babu Dula dakika ya 88 baada ya kupokea pasi safi toka kwa Anusa Kasembe.
Huku uwanja wa Nangw'anda mkoa Mtwara Ndanda FC na Green Warriors walitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya kufungana 2-2.
Uwanja wa Samora mjini Iringa, Pilisi Iringa walitoshana nguvu na Mbeya City kwa kutoka sare baada ya majuzi mchezo kuahirishwa kutokana na mvua iliyonyesha mkoani Iringa
Kesho ligi hii itaendelea kwa polisi Dar es salaam kucheza na Moro Utd uwanja wa Karume
No comments:
Post a Comment