TIMU ya wasichana chini ya umri wa miaka 16 ya mchezo wa kikapu ya Tanzania imeibuka mabingwa wa mashindano ya Kanda ya Tano Afrika yaliyokuwa yakichezwa katika Kituo cha Michezo cha Filbert Bayi, Kibaha mkoani Pwani.
Mashindano hayo
yalianza Juni 12 na kumalizika juzi yakishirikisha timu za wasichana na
wavulana kutoka Kenya, Burundi na Tanzania.
Tanzania iliibuka
bingwa baada ya kuifunga Kenya kwa pointi 71-69 na kuifunga Burundi kwa pointi
88-17 wakati Kenya waliifunga Burundi kwa pointi 90-15.
Katika michezo ya
wavulana Tanzania ilishika nafasi ya pili wakati mabingwa wakiwa Burundi na
Kenya mshindi wa tatu.
Burundi waliifunga
Tanzania 65-53, Kenya 80-66 na Tanzania iliifunga Kenya 64-62.
Kwa upande wa mchezaji
mmoja mmoja wasichana Tanzania ilitoa 'best pointer' ambaye ni Magdalena Mollel
na Namnyak Mollel akiibuka 'best rebounder'.
Kwa upande wa
wavulana, Tanzania ilitoa 'best rebounder', Farabi Kanyungilo na mfungaji bora,
Venance Kikasa.
No comments:
Post a Comment