Na Rahel Pallangyo
SERIKALI imepongeza uongozi wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuingia mkataba wa miaka mitano na Kampuni ya Sandaland Fashion Wear LTD
wenye thamani ya Sh bilioni 3 kwa ajili ya kuzivalisha timu zote za Taifa.
Pongezi hizo
zilitolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas
Ndumbaro, Dar es Salaam juzi baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo.
“Nashukuru sana uongozi wa TFF chini ya uongozi wa
ndugu yangu Wallace Karia, ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi
hii, TFF inaingia mkataba na mtengenezaji jezi kwa ajili ya timu zote za Taifa,
tunaweza kulichukulia jambo hilo kama dogo sana lakini halijawahi kufanyika na
linafanywa na TFF chini ya jemedari Wallace Karia,”
“Nasisitiza haya kwa sababu sisi Watanzania ni
wazuri sana wa kukosoa lakini tunakuwa wachoyo kusifia pale jambo zuri
linapofanyika na kwa mara ili timu zote za taifa ziwezi kupata jezi rasmi
zinazotengenezwa na kampuni yenye heshima kubwa hapa Tanzania,” alisema Dk
Ndumabaro.
Naye Rais wa TFF Wallace Karia alisema mkataba huo
utahusisha timu zote za Taifa na katika mkataba huo watakuwa wanapewa jezi bure
kwa timu zote na watakuwa wanapata fedha.
“Leo tunatimiza ahadi yetu ya kuongeza wadhamini
zaidi. Mkataba huu ni wa kihistoria kwani tutakuwa tunapata jezi bure na pia
tunapata fedha jambo halijawahi kutokea,” alisema Karia.
Pia Karia alisema huo ni utekekezaji wa maagizo ya
Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka wawekezaji wazawa kupewa nafasi zaidi ambapo
alisema atakuwa anawalegezea kwenye kodi.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Sandaland Fashion Wear LTD, Yusuph Yenga
alisema kampuni hiyo ina uzoefu wa kutengeneza jezi na kuahidi kuwa jezi hizo
zitakuwa na ubora na viwango vya hali ya juu.
Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani (FCC),
William Erio alipongeza TFF kwa mafanikio waliyopata katika kipindi cha uongozi
wa Karia.
“Sisi Tume ya ushindani ni kuhakikisha
wafanyabiashara wanafanikiwa kwa kuweka mazingira mazuri na nimefurahi kuona
kampuni ya wazawa imeshinda zanuni ya kutengeza jezi za timu za Taifa,”
No comments:
Post a Comment