Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 19, 2023

MAJALIWA MGENI RASMI NBC MARATHON 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi wakionyesha jezi za kukimbilia muda mfupi baada ya kutangaza kukamilika kwa maandalizi yam bio za NBC Dodoma Marathon 2023 zitakazofanyika Jumapili, Julai 23. Mbio hizo zinalenga kukusanya shilingi milioni 500 kwa ajilya kusaidia mapambano dhidi ya kansa ya shingo ya kizazi nan a kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika mbio za NBC Dodoma Marathon 2023 zinazotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili Julai23 2023. Mbio za mwaka huu zinalenga kukusanya jumla ya shilingi milioni 500. Fedha hizo zitatumika kusaidia kupambana na kansa ya shingo ya kizazi pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wakunga ikiwa ni sehemu ya kusaidia kuongeza wataalamu ili kupunguza vifo vya uzazi. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya mbio hizo zilizojizolea umaarufu mkubwa na ambazo zinafanyika kwa mara ya nne mfululizo mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule alisema mkoa umejipanga vyema kuwapokea wakiambiaji na wageni wote wataoshiriki. “Kwanza kabisa napenda kuishukuru benki ya NBC kwa kuandaa mbio hizi zenye faida kubwa kwetu kama nchi. Pili niwahakikishie washiriki wote kuwa sisi kama mkoa wa Dodoma tumejipanga vyema kuwahudumia na kuwafanya wafurahie ujio wao hapa Dodoma pamoja na ushiriki katika mbio za mwaka huu,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi alisema mbio za mwaka huu pamoja na kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi zitasaidia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutoa ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wanaosomea taaluma ya ukunga ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi. “Kupitia mbio hizi za NBC Dodoma Marathon 2023, tunalenga kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi kupitia kusaidia kwenye mapambano vifo vinavyoweza kuepukika na ambavyo vinatokana na uzazi kupitia kusaidia kupata wataalamu zaidi ktika eneo hili. Tunaamini kupitia mbio hizi tutaweza kuisaidia jamii yetu kupambana na changamoto hii ambayo inaathiri maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla,” alisema Aliongeza “Vilevile tunaendelea na msaada wetu katika mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi. Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 500 zilizosaidia kufikia upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake zaidi ya 23,500 na matibabu kwa zaidi ya wanawake 1,300. Tunajivunia mafanikio haya” alisema. Mkurugenzi huyo aliwataka Watanzania wote kujitokeza katika mbio hizo ili kujenga faya zao kupitia zoezi la kukimbia lakini wakati huo huo wakisaidia kupambana na saratani ya shingo ya kizazi pamoja na kusaidia kupunguza vifo vya uzazi. Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri aliishukuru NBC kwa kuiamini wilaya ya Dodoma na kuamua kufanyia mbio hizo wilayani hamu huku akiwahakikishia kuwa maandalizi yamekamilika kufanya mbio hizo kuwea zenye mafanikio.

No comments:

Post a Comment