Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 27, 2018

MWAMUZI NKONGO AUNDIWA KAMATI KUANGALIA UWEZO WAKE

KAMATI ya uendeshaji wa ligi imeteua wajumbe watatu kuchunguza kiwango cha uchezeshaji cha mwamuzi Israel Nkongo na kuwasilisha taarifa yake kwa ajili ya hatua zaidi.
Akizungumza  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi (TPBL) Boniface Wambura alisema kuwa Nkongo alichezesha mchezo dhidi ya Mbeya City na Kagera na kumalizika kwa sare ya 1-1 licha ya kuwa hakuna timu iliyolalamika kamati imeamua kufanya hivyo ili ichukue hatua stahiki.
“Kamati hiyo itapitia mkanda wa mechi hiyo na kuchunguza kiwango cha uchezeshaji cha Nkongo na kuwasilisha taarifa kwa ajili ya hatua stahili maana baada ya mchezo kumalizika mashabiki walitaka kumpiga lakini askari waliwadhibiti,” alisema Wambura
Katika mchezo huo Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyochezwa Januari Mosi, 2018, Mbeya, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu na adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49).
Kocha wa Mbeya City, Ramadhani Mwazurimo amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na kosa la kuondolewa kwenye benchi na mwamuzi baada ya kumtolea lugha ya kashfa katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 14, 2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mbeya.
Pia klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwa madai alikataa kutoa penalti kwa timu hiyo.
Azam FC imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na kukataa wachezaji wake wakaguliwe ndani kwa madai kuwa chumba kimepuliziwa dawa katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 18, 2018 Uwanja wa Majimaji mjini Songea na wamepewa siku saba kuthibitisha madai yao.


Mtunza Vifaa wa Singida United FC, Mussa Rajab amefungiwa mwezi mmoja na kupigwa faini ya sh. 300,000 kutokana na kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mapumziko na kumlalamikia mwamuzi wakati wa mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Taifa Januari 18.

No comments:

Post a Comment