Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 26, 2018

LEO NDIO LEO LIGI DARAJA LA KWANZA KUNDI A NA KUNDI C

PRESHA inapanda na kushuka kuelekea lala salama ya Ligi Daraja la Kwanza kwa timu za Friends Rangers, African Lyon, zinazotafuta nafasi moja kupanda Ligi Kuu, huku Ashanti na Mvuvumwa zikipigania kutoshuka daraja Kundi A.

Tayari JKT Tanzania imekata tiketi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao kutoka katika Kundi A baada ya kucheza michezo 12, kufikisha pointi 31, ambazo haziwezi kufikiwa na yeyote katika michezo miwili kila mmoja aliyobakiza.

Mchezo wa leo, JKT Tanzania dhidi Friends Rangers kwenye Uwanja wa Mbweni, utatoa taswira baada ya matokeo.

Lakini presha itakuwa kubwa hasa kwa Rangers yenye pointi 22 kutafuta matokeo mazuri ingawa JKT imekuwa ni timu ngumu kufungika hasa kwenye uwanja wake.

Pia, kazi ni kubwa zaidi kati ya Ashanti United dhidi ya African Lyon kwa kuwa zote zitapigana kupata matokeo mazuri, Lyon ikitafuta nafasi ya kupanda Ligi Kuu na Ashanti ikipigania kutoshuka daraja.

Lyon ina pointi 21 tofauti ndogo na Rangers na zote kila mmoja anamuombea mwenzake mabaya, mmoja akishinda michezo hiyo na ile ya mwisho ni faida kwa mwingine, zikitoka sare au kupoteza kazi itakuwa nzito na pengine zikija kulingana pointi tofauti ya mabao itaamua baada ya mchezo wa mwisho.

Ashanti United ina pointi tisa na Mvuvumwa pointi nne, hivyo kushuka kwao kutategemea na nani amemzidi mwenzake baada ya michezo miwili ya mwisho.

Mvuvumwa ikifungwa ugenini kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga dhidi ya Mgambo Shooting yenye pointi 15, itajiweka kwenye hatari zaidi ya kushuka daraja. Hata ikishinda pia, haisaidii labda imuombee Ashanti ipoteze michezo yote na yeye ashinde  ndiyo atanusurika.

Mgambo, Mshikamano zenye pointi sawa 15 na Kiluvya yenye pointi 17 hata zikipata matokeo mazuri hazishuki wala hazipandi. Mshikamano itachuana dhidi ya Kiluvya United. Ingawa Kiluvya itakuwa ina nafasi kama Lyon na Friends Rangers zitafungwa michezo yote ya mwisho.

Katika mechi za Kundi C, ambazo zitachezwa pia leo, kazi ipo kubwa kwa Biashara, Alliance na Dodoma FC,  ambapo timu mbili za kwanza ndizo zitapanda daraja.

Kinara wa kundi ni Biashara yenye pointi 24, Alliance yenye pointi 22  sawa na Dodoma yenye pointi 22, huku Toto Africans, Pamba, Transit Camp na Oljoro zikipigania kutoshuka daraja.

Biashara itacheza leo dhidi ya Oljoro mchezo ambao ni mgumu ikiwa kwenye uwanja wa ugenini Moshi kwa kuwa kila mmoja atakuwa ana kazi ya kutafuta pointi za kumwezesha kufikia malengo yake.

Alliance ina nafasi ya kufanya vizuri kama itatumia vyema uwanja wake wa nyumbani kupata matokeo mazuri ila bado hautakuwa rahisi kwa sababu Pamba inataka matokeo kupigania nafasi ya kutoshuka daraja.

Dodoma pia, ina nafasi ya kufanya vizuri kama itatumia vyema uwanja wake wa nyumbani kupata matokeo dhidi ya Trans Camp lakini vile vile, Camp inahitaji matokeo kujihakikishia nafasi ya kutoshuka daraja, na Toto Africans isipojitahidi dhidi ya Rhino Rangers iko hatarini zaidi kushuka kwani ndiyo inayoshikilia mkia.

No comments:

Post a Comment