Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 30, 2017

GEORGE WEAH HATIMAYE ZIMETOSHA

Image result for george weah
*Wapo marais wanaosakata soka hadi sasa
Monrovia (AFP) –

MWANASOKA bora wa zamani wa Dunia George Weah ametangazwa kuwa rais wa Liberia baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa taifa hilo alhamisi hii, akimpita kirahisi mpinzani wake Joseph Boakai.

"Wananchi wenzanngu wa Liberia, nahisi hisia za taifa zima. Napima umuhimu wa 
wajibu na majukumu yangu kwenu kwa ushindi huu. Mabadiliko yanakuja,”alisema Weah kwenye akaunti yake ya Twitta.
Mamia ya mashabiki wake walikuwa wakizunguka kwenye mitaa ya jiji la Monrovia kushanglia ushindi wa mwanasoka huyo nyota wa zamani wa klabu za Monaco, Paris Saint-Germain, Ac Milan, Chelsea na Manchester City.

"Sikuwa na furaha kwenye maisha yangu yote. Tulikuwa wapinzani kwa miaka 12.Tunaenda kuweka historia, kama ambavyo watoto wa Afrika Kusini waliwahi kufanya.
 Hivyo nina furaha sana," alisema Josephine Davies, mgombea mwenza wa George Weah katika chama  Congress for Democratic Change.
"Tulisubiri kwa miaka 12, sasa nguvu inarudi kwa wananchi."

Weah, mwenye umri wa miaka 51 anachukua nafasi ya  Ellen Johnson Sirleaf, ambae aliiongoza Liberia tangu mwaka 2006.
Tume ya Uchaguzi ya taifa hilo ilisema Weah alishinda kwa asilimia 61.5  ambapo matokeo hayo yalicheleweshwa kwa wiki kadhaa akimshinda mpinzani wake Joseph Boakai.
Tume hiyo ya uchaguzi ilisema kati ya asilimia 98.1 ya kula zote zilizohesabiwa, Boakai alipata asilimia 38.5.
Bottom of Form

UNAPOSIKIA majina ya wacheza soka wa zamani kama vile Pele (Edson Arantes do Nascimento), Diego Maradona, Zinedine Zidane au wa sasa Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Neymar na Mohamed Salah, ujue kuna wengine wengi nyuma yao.
Hao ni pamoja na Rais mteule wa Liberia, George Weah, ambaye baada ya safari ndefu ya milima na mabonde kwenye siasa za nchi hiyo kwa zaidi ya muongo, na uchaguzi wa mwaka huu kuingia raundi mbili, hatimaye ameukwaa urais.

Anaweka historia barani Afrika kwa kuwa Rais wa kwanza aliyekuwa mwanasoka, na kwa namna ya pekee ni mchezaji aliyepata kutwaa tuzo ya mwanasoka bora duniani, nayo ilikuwa 1995 akiwa wa kwanza kutoka Afrika kupewa tuzo hiyo – Ballon d’Or.  Weah alikuwa akikikipiga nafasi ya ushambuliaji na ni mmoja wa waliotokea kuwa wakali zaidi wa zama zake.

Wakati mwaka 1989 na 1994 sawa na 1995 alichaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika, mwaka uliofuata alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika wa Karne. Alitambulika zaidi kwa kasi yake ya kukokota mpira na ufungaji mabao bora kabisa. Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) linamtaja kama mtu ambaye ingekuwa leo, basi angefanya kazi za washambuliaji kadhaa.

Leo hii wapo viongozi wengine wanaocheza soka, lakini si ile kali ya kiushindani, japokuwa nayo ni soka tu, na wana pumzi ya kutosha. Nitawataja wawili, nao wanatoka Afrika Mashariki, wakiwa ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Sasa tuwaone watu waliocheza soka kisha wakaja kuwa viongozi wakubwa kisiasa au kidini, mmoja akawa kiongozi wa kanisa mojawapo dunia nzima.

PAPA YOHANA PAULO 11
Akiwa mvulana mdogo huko kwao Wodowice, Poland, Karol Jozef Wojtyla, alikuwa mchezaji mzuri wa soka katika klabu yao ndogo ya shule na kidini. Huyu ndiye aliyekuja kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Yohana Paulo II ambaye amefariki dunia na tayari ametangazwa kuwa Mtakatifu.
Huyu amepata kudumisha amani baina ya timu za jamii tofauti, akijitolea kucheza upande wa Wayahudi, pale walipokuwa wakicheza dhidi ya Wakatoliki na ikatokea kwamba Wayahudi hawakuwa na idadi ya kutosha ya wachezaji. Licha ya kufuata wito wa upadre na kupanda hadi kuwa Baba Mtakatifu, Yohana Paulo II alibaki na mapendo kwa soka na huko Brazil kuna uwanja unaitwa kwa jina lake - Estádio João Paulo II.

EVO MORALES
Evo Morales ni nani? Ndiye Rais wa sasa wa Bolivia aliyecheza sana soka enzi zake. Akiwa na umri wa miaka 14, Morales alionesha ukomavu wa kiuongozi baada ya kuandaa kundi la wanasoka, akawa kocha wao na mchezaji pia, na kikosi kikawa kizuri chenye ushindani mkubwa kilichocheza kwenye jimbo zima analotoka.
Akiwa na umri wa miaka 16, Morales alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa kikosi hicho kilichoingia katika ligi ndogo ya eneo lao, na mwaka 1981 akiwa na umri wa miaka 22 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha soka cha eneo lao.
Japokuwa Morales aliamua kufuasa siasa na kujitolea kwa kile anachokiita kuboresha maisha ya watu wake, anaendelea kucheza soka kila akipata nafasi popote pale nchini mwake. Jamaa huyu aliyetokea kuwa pia mjumbe wa chama cha wafanyakazi mwenye siasa za mrengo wa kushoto, anaipenda soka na hupenda kuwezesha watu kuicheza. 

FERNANDO DE MELLO 
Fernando Collor de Mello alihudumu kama rais wa 32 wa Brazil. Alitumikia Ikulu kwa miaka miwili, akajiuzulu 1992 kama njia mojawapo ya kukwepa kushitakiwa akiwa madarakani, mashitaka yaliyokuwa yameletwa dhidi yake na serikali ya taifa lake.
Huyu alikuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa kwa uhuru na demokrasia ya uwazi baada ya kipindi cha utawala wa kijeshi. De Mello alicheza soka sana muda wote wa ujana wake na akatumia soka kama jukwaa lake au manati ya kumfanikishia mambo ya siasa.
Akiwa na umri wa miaka 27 tu, De Mello alikuwa rais wa klabu ya Centro Sportivo Alagoano, akatumia umaarufu aliojikusanyia kuwania na kutwaa nafasi ya meya wa Jimbo la Alagoas. Kwa sasa si mtu anayeenziwa sana nchini Brazil, kwa sababu alichaguliwa kwa ajili ya kudhibiti rushwa, lakini anadaiwa badala yake aliungana na wala rushwa, kama si kuwazidi kwa kuila badala ya kuimaliza.

 OSAMA BIN LADEN 
Kiongozi wa zamani wa genge la kigaidi la Al Qaeda, Osama Bin Laden ni mtu aliyekuwa na mahaba makubwa na soka, akijadiliwa kwamba alikuwa shabiki mkubwa wa Arsenal, lakini haikuwa tu imeelezwa kama alicheza. Sasa chukulia kwamba alicheza enzi za utoto na ujana wake.
Hakucheza soka ya kulipwa bali ile ya ridhaa, akawa huko sana, na inaelezwa kwamba ni kutoka huko aliwachagua makamarada wake kwa ajili ya mambo yake ya kupigania aliyoyaamini baadaye, akiwapeleka nje ya nchi.

BOB MARLEY
Bob Marley hakuna kumfyatua Mzungu ubavuni, hakuna kumfyatua Mwafrika ubavuni, bali yeye aliufyatua mpira huko uwanjani. Bob alikua akicheza soka nchini Jamaica akiwa shule lakini pia nje ya shule katika ligi za mikoa na majimbo yao.

Baba yake alikuwa Mwingereza na mama Mjamaica, akasema soka ilikuwa kwenye damu yake, lakini baadaye akajikita zaidi kwenye muziki, japo kuna video zake za muziki akicheza soka pia.
 Alibobea kwenye muziki kwas ababu enzi zile hapakuwapo fursa za kucheza soka ya kulipwa huko Caribbean. Zipo picha nyingi mithili ya mabango, ya Bob, akicheza soka, hata kwenye migahawa Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha.

No comments:

Post a Comment