Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 15, 2017

NDIKUMANA MUME WA IRENE UYOWA AFARIKI JANA USIKU

MSANII wa Bongo Muvi, Irene Uwoya amesema ni kipindi kigumu kwake kuondokewa na aliyekuwa mume wake, Hammad Ndikumana Katauti.

Habari za kifo cha Ndikumana zilianza kusambaa jana asubuhi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram.

Gazeti hili lilizungumza na Uwoya ambaye anaomboleza msiba wa mzazi mwenzake nyumbani kwake Sinza Mori, Dar es Salaam na kusema: “ Imeniuma, Hammad ni mzazi mwenzangu, baba wa mtoto wangu, pamoja na tofauti zetu, bado ni baba wa mwanangu mpendwa, ”alisema Uwoya  huku akiangua kilio na watu mbali mbali wakiwemo wasanii wa filamu walikusanyika nyumbani kwa msanii huyo.

Alisema anangalia utaratibu ili yeye na mtoto wake waweze aweze kwenda kuhani msiba wa mumewe huyo wa zamani ambaye ni mzaliwa wa Burundi, lakini alicukua uraia wa Rwanda.

Ndikumana alifunga ndoa ya kikristo na Uwoya mwaka 2009 na  kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la Krish, lakini ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu wakatengana, ambapo hivi karibuni kulitoka taarifa kwa Irene kufunga ndoa na  Abdulaziz Abubakari ‘Dogo Janja’.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Rayon Sports ya Rwanda, Gakwaya Olivier alisema Ndikumana  ambaye alikuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo alifariki ugonjwa wa moyo.

Akizungumzia msiba huo, kiungo wa Simba ya Dar es Salaam, ambaye ni raia wa Rwanda, alisema: “Pumzika kwa amani kaka Ndikumana, tumekupenda ila Mungu amekupenda zaidi, hakika umetuachia majonzi makuu.”

Naye mshambuliaji wa Yanga ya Dar es Salaam, Amiss Tambwe ambaye ni raia wa Burundi, alisema: “Nasikitika kwa kifo cha Ndikumana, yani simani kabisa kama amekufa, hakika kifo hakina huruma. Amekufa bado mdogo.”

Jana mitandao ya kijamii suala al kifo cha Ndikumana lilikuwa gumzo kwa wengi kuonesha mshtuko wa nini kimemkumba nyota huyo wa soka hadi mauti hayo kumkumba.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii walikuwa wakituma ujumbe wa kumtakia apumzike kwa amani Ndikuma na kusema wanaadamu wote njia yao ni moja.


Ndikumana ambaye alikuwa na umri wa miaka 39 amechezea timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na nchini Ubelgiji na Cyprus, ambapo mwaka 2015 alisajiliwa na Stand United ya Shinyanga inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, ingawa alikaa muda mfupi.

No comments:

Post a Comment