Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 15, 2017

HALMASHAURI YA NAMTUMBO KUENDESHA TAMASHA LA MUZIKI

Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma katika harakati yake ya kuhakikisha wanajenga kituo cha Redio ya jamii katika Halmashauri hiyo imepanga kuanzisha Tamasha la muziki kwa lengo la kupata fedha kujenga kituo cha Redio.
Kamati ya uanzishwaji Redio katika Hamashauri hiyo imependekeza kuundwa kwa kamati ndogo itakayoratibu kuanzishwa kwa Tamasha la muziki kwa lengo la kuchangia ujenzi wa kituo hicho cha Redio.
Aidha mwenyekiti wa kamati ya uanzishwaji Redio ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Gwakisa Mwasyeba ambaye ni Afisa mipango wa Halmashauri hiyo alipendekeza majina ya kamati hiyo kuwa ni James komba Afisa utamaduni wa wilaya hiyo , Afisa manunuzi Robert Mahili, Abbas Masawe katibu wa mikutano ya madiwani , na Afisa michezo John Ligoho na kuwataka kuanza mikakati ya kuanzishwa kwa Tamasha hilo la muziki.
Hata hivyo kamati ya uanzishwaji Redio ya Halmashauri hiyo ilipendekeza Hadidu Rejea kwa kamati hiyo ndogo ili zianze kushughulika nazo na kutoa taarifa kamili kwenye kamati kuu ya uanzishaji Redio .

No comments:

Post a Comment