Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa Oktoba 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa
wenyeji Yanga kushinda mabao 3-2 limeingiza sh. 47,615,000.
Watazamaji
8,233 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 8,420,578.47 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 7,263,305.08.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000,
kamishna wa mechi sh. 203,000, waamuzi sh. 381,000, mwamuzi wa akiba sh.
70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium
technical support) sh. 2,000,000.
Umeme
sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000,
ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 2,959,100. Gharama za
mchezo sh. 2,806,859.49, uwanja sh. 2,806,859.49, Kamati ya Ligi sh.
2,806,859.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,684,115.69 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 1,122,743.80.
No comments:
Post a Comment