Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 18, 2014

Orodha mpya ya viwango vya soka duniania baada ya kombe la dunia Ujerumani inaongoza,Uholanzi, Ubelgiji na Costa rika zapaa, Brazil yaanguka sana Tanzania mwendo ni ule ule.


Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kinacho ongoza kwa ubora wa viwango vya FIFA
Kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kilicho shika nafasi ya pili kwa ubora

Wenyeji wa fainali za kombe la dunia 2014 Brazil washika nafasi ya saba kwa ubora wa FIFA

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kikishika nafasi ya 106 duniani

Shirikisho la soka duniani FIFA, hii leo limetangaza orodha ya viwango vya ubora wa soka, ikiwa ni juma moja baada ya kukamilika kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 huko nchini Brazil.
Orodha hiyo ambayo hutolewa kila mwezi, imezingatia matokeo ya michezo ya fainali za kombe la dunia, ambapo mataifa makubwa kama Uingereza yameonekana kutupwa mbali.
Wenyeji wa fainali za kombe la dunia Brazil nao wameonekana kuanguka kwa kiasi kikubwa, ili hali waliokuwa mabingwa wa fainali hizo mwaka 2010 Hispania wameporomoka kwa kasi ya ajabu wakitokea nafasi ya kwanza.
Mabingwa wapya wa fainali za kombe la dunia, Ujerumani wamekalia kiti cha orodha hiyo, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa walipokuwa nchini Brazil, ambapo walicheza michezo saba pasina kufungwa mchezo wowote.
Ifuatayo ni orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani kwa mwezi July mwaka 2014.
1. Ujerumani (+1)
2. Argentina (+3)
3. Uholanzi (+12)
4. Colombia (+4)
5. Ubelgiji (+6)
6. Uruguay (+1)
7. Brazil (-4)
8. Spain (-7)
9. Uswisi (-3)
10. Ufaransa (+7)
11. Ureno (-7)              
12. Chile (+2)               
13. Ugiriki  (+1)           
14. Italia (-5)                
15. Marekani  (-2)                  
16. Costa Rica (+12)             
17. Croatia (+1)          
18. Mexico (+2)          
19. Bosnia na Herzegovina (+2)              
20. Uingereza (-10)      
AFRIKA MASHARIKI NA KATI
87. Uganda (-1)
95. Kenya (+13)
96. DRC (-12)
106. Tanzania (+7)
109. Rwanda (+7)
126. Burundi (+2)

No comments:

Post a Comment