Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 23, 2017

MBEYA, KATAVI, SONGWE NA RUKWA KUNUFAIKA NA KOZI YA GRASSROOTS






KOZI ya Grassroots kwa Vijana kuanzia miaka 6-12, inatarajiwa kufanyika mkoani Mbeya kuanzia Novemba 27, hadi Desemba Mosi, mwaka huu.
Akizungumza Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi alisema kozi hiyo itahusisha walimu wa Shule za Msingi za mikoa ya Songwe, Katavi, Rukwa na wenyeji Mbeya.
“Jumla ya washiriki 30 watahudhuria kozi hiyo na kila mkoa utatoa washiriki saba isipokuwa wenyeji Mbeya watatoa washiriki tisa,” alisema Madadi
Kozi hiyo imezingatia jinsia kwa kila mkoa unatakiwa kutoa idadi sawa au wanawake wawe wengi zaidi ya wanaume ili kutoa hamasa zaidi kwa wanawake kujifunza.
Kozi hiyo ya Grassroots itakwenda sambamba na Kampeni ya ‘Live Your Goal’ ikiwa na maana ya ‘Ishi ndoto zako’ itayofanyika Novemba 29, ikiwa na lengo la kutoa hamasa kwa soka la wanawake.
Kampeni hiyo ya Live Your Goal inalenga kutoa hamasa kwa wadau waujue, waupende na kuheshimu soka la wanawake kama ilivyo kwa upande wa wanaume na itachezwa mechi na timu za wanawake za mkoa wa Mbeya.
Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA), Elias Mwanjala amewakaribisha washiriki watakaohudhuria kozi na kusema wapo tayari kupokea ugeni huo kwa maendeleo ya mpira wa miguu.
Mpango wa Grass roots kabla ya kwenda kufanyika Mbeya ulifanyika huko Mkoani Lindi.


No comments:

Post a Comment