Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 23, 2017

KOCHA AZAM KUKOSA MECHI TATU NA FAINI JUU

KAMATI ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imemfungia kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba kwa mechi tatu na faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kuwabughudhi waamuzi katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting iliochezwa Novemba 4, 2017 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam
Akizungumza leo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema Cioaba aliwafuata waamuzi na kuwalalamikia kwa kurusha mikono akionyesha kutoridhika na maamuzi yao.
Adhabu ya Cioaba imezingatia Kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha na Tanzania Prisons imepewa onyo kali kwa kuwakilishwa kwenye benchi na ofisa tofauti na yule aliyeudhuria kikao cha maandalizi,” alisema Wambura. 
Wambura alisema Tanzania Prisons iliwakilishwa na Meneja wake Erasto Ntabah lakini kwenye benchi alikaa Hassan Mtege katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Novemba 4 kwenye Uwanja wa Kaitaba Kagera

“Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo na Ntabah amesimamishwa hadi suala lake la kutoka jukwaani na kwenda kumfokea mwamuzi wa akiba litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF,” alisema Wambura
Pia Wambura alisema mchezaji wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko kwenye paji la uso mchezaji wa Kagera Sugar.
Hata hivyo uongozi wa Azam FC umesema unasikitishwa na kitendo cha Kamati hiyo kumfungia kocha Cioaba bila kuwapa taarifa.

“Tunasikitika kusikia habari za kufungiwa kocha kupitia vyombo vya habari, tulipaswa kutaarifiwa kiofisi kabla ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari,” alisema Msemaji wa Azam FC, Jaffa Idd.

No comments:

Post a Comment