Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 23, 2017

KARIA AJITOSA CECAFA

Image result for KARIA WALLACE
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) unaotarajiwa kufanyika Desemba 2, mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili kutoka Nairobi jana, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema Karia atawania nafasi ya mjumbe wa kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Nairobi siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Chalenji.
Michuano ya Chalenji imepangwa kuanza Desemba 3- 17 ambapo timu 10 zinatarajiwa kushiriki.
“Maandalizi ya uchaguzi yamekamilika na wagombea wa nafasi hiyo wapo wanane kutoka nchi wanachama.
Musonye aliwataja wagombea wengine ni Abdigaani Said wa Somalia, Moses Magogo wa Uganda, Juneid Basha kutoka Ethiopia, Aimabale Habimana wa Burundi na Rais wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), Vincent Nzamwita.
Karia anafuata nyayo za rais wa zamani wa TFF Leodegar Tenga aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Cecafa.
Kwa sasa mwenyekiti wa Baraza hilo ni Gaffar Mutasin wa Sudan.
Musonye alisema uchaguzi wa mwaka huu pia kuna wanawake wawili wanaowania nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji ya Baraza hilo.
Aliwataja wanawake hao ni Doris Petra wa Kenya na Kourecha Guedi wa Djibouti.
“Tumefurahi kwamba sasa wigo unapanuka kwenye kamati yetu ya Utendaji tutakuwa na wanawake ikitokea watachaguliwa,” alisema.
Musonye alisema, baada ya uchaguzi kutakuwa na mkutano mkuu wa mwaka wa Baraza hilo ambao utahudhuriwa na wenyeviti na makatibu wakuu wa nchi 12 wanachama.
“Baada ya mkutano huo, sasa mashindano ya Chalenji yataanza rasmi ambapo tunatarajia yatakuwa ya kupendeza msimu huu,” alisema.
Michuano ya Chalenji inafanyika baada ya mwaka jana kutofanyika. Mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2015, Addis Ababa, Ethiopia ambapo Uganda ilitwaa ubingwa.

Baada ya mkutano huo, mashindano ya kuwania Kombe la Chalenji ambayo mwaka huu yanashirikisha timu 10 yataanza rasmi kufanyika.

No comments:

Post a Comment