Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 6, 2012

LIGI KUU TANZANIA BARA, AZAM YAZIDI KUPAA YAICHAPA LYON CHAMAZI. COASTAL UNION TAABANI KWA RUVU SHOOTING.

 
Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imendelea tena leo kwe michezo miwili kuchezwa katika viwanja viwili tofauti.
Katika uwanja wa Azam Complex kule Chamazi Azam fc imefanikiwa kupata points zote tatu muhimu baaada ya kuifunga Afrikan Lyon kwa bao 1-0 lililofungwa na John Boko baada ya kupata pasi ya Kipre tcheche aliyeunasa mpira uliomtoka mlinda mlango wa Lyon.
Matokeo hayo yameifanya Azam kufikisha jumla ya points 13 sawa na Simba ambao ndio mabingwa watetezi wa taji la ligi hiyo na ambao kesho watakuwa wakishuka dimbani kucheza dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo mwingine uliochezwa leo ni baina ya Ruvu Shooting ya Pwani waliokuwa wenyeji wa Coastal Union ya Tanga mchezo ambao umefanyika katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Katika mchezo huo wenyeji JKT Ruvu wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0, matokeo ambayo yamewafanya Ruvu kufikisha jumla ya points 9 na hivyo kukalia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment