Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 23, 2017

KMC YAPOKWA POINTI KWA UZEMBE KAMA MSIMU ULIOPITA

TIMU ya KMC imepokwa pointi tatu na mabao matatu na kupewa JKT Mlale kwa kosa la kumchezesha mchezaji Stephano Mwasika katika mechi wa ligi daraja la kwanza uliochezwa Oktoba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salam

Akizungumza leo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alisema Mwasika alikuwa na adhabu ya kadi nyekundu ambayo alitakiwa kukosa michezo mitatu na kulipa faini ya sh. 300,000
“Mwasika alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko mpinzani wake kwenye mechi dhidi ya Mbeya kwanza iliyochezwa Oktoba 5, 2017 katika Uwanja wa Azam Complex na alipaswa kukosa michezo mitatu lakini yeye amekosa michezo miwili tu,” alisema Wambura.

Katika mchezo huo ambao Mwasika alicheza dhidi ya JKT Mlale uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, KMC ilifikisha pointi 19, hivyo kuondolewa kwa pointi za mchezo huo inabaki na pointi 18 kileleni mwa kundi B ikifuatiwa na Polisi Tanzania yenye 16 na JKT Mlale, Mbeya Kwanza na Coastal Union ambazo zinawania nafasi ya tatu zikiwa na pointi 15.
Hii ni mara pili kwa KMC kupokwa pointi baada ya msimu uliopita kupokwa kwa kosa la kufanya mabadiliko ya wachezaji wanne badala ya watatu katika mchezo mmoja.
Nayo JKT Mlale imepigwa faini ya sh. 200,000 kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi  dhidi ya Coastal Union na Mvuvumwa imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kosa la kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi dhidi ya African Lyon ikiwa na maofisa pungufu.
Coastal Union imepewa onyo kali kutokana na kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu na Toto Africans imepewa onyo kali kutokana kuchelewa kikao cha maandalizi pamoja na waamuzi Jumanne Njige na Bam Bilasho kwa kuchezesha mechi chini ya kiwango.


Meneja wa Toto Africans, Yusufu Jumaa amefungiwa miezi miwili na kupigwa faini ya sh. 200,000 wakati mtunza vifaa wa JKT Mlale, Noel Murish na Ofisa Habari wa Toto Africans, Cuthbert Japhet hadi masuala yao yatakaposilikizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.

No comments:

Post a Comment