Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, November 23, 2017

TANZANIA YAPOROMOKA FIFA


TANZANIA imezidi kuporomoka kwenye viwango vya ubora vya Fifa na sasa inashika nafasi ya 142 kutoka nafasi ya 136 iliyokuwa mwezi uliopita.
Kuporomoka huko kumekuja siku chache baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Benin mwanzoni mwa mwezi huu, matokeo ambayo yalitoa matumaini kwa wengi kwamba huenda ikapanda kwenye viwango hivyo.
Kwa mujibu wa orodha ya viwango hivyo iliyotolewa kwenye tovuti ya Fifa jana, Benin iko nafasi ya 82.
Kwa upande wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeendelea kuongoza kama ilivyo siku zote ikiwa nafasi ya 74.
Kwa upande wa Afrika, Senegal ndio inayoongoza ikiwa nafasi ya 23 ikifuatiwa na Misri nafasi ya 31.
Ujerumani imeendelea kukaa kileleni katika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.


No comments:

Post a Comment