Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, September 4, 2017

TASWA ARUSHA KUFANYA BONANZA NYERERE DAY

Related image
Katibu wa TASWA-ARUSHA Mussa Juma wa nne kutoka kulia akiwa  pamaoja na wadhamini wa muda mrefu wa bonanza la wanahabari mkoani Arusha mara baada ya kumaliza mkutano na wanahabari ambapo wametangaza kuwa bonanza la mwaka huu litafanyika siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere 
Image result for media bonanza arusha










 

Waandishi wa Habari kutoka chuo cha uandishi wa Habari Arusha wakifurahia ushindi wao katika moja ya mabonanza yaliyopita jijini Arusha ambapo chuo hicho kimekuwa kikishriki bonanza hili toka mwaka 2008 na mwaka huu wamethibitisha kushiriki tena
Wakufunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia mwenendo wa Mchezo kati ya Sunrise Redio na  Chuo cha AJTC 




Mwandishi wetu,Arusha

Wanahabari zaidi ya 400 wanatarajia kushiriki katika Tamasha   la vyombo vya habari, Kanda ya kaskazini, litakalofanyika kuanzia Octobar 14 siku ya kumbukumbu ya mwalimu Julius Nyerere hadi octobar 15 mwaka huu.

Siku ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere kutakuwa na kongamano  kujadili mchango wa hayati baba wa Taifa, katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na michezo na baadaye octobar 15 kutakuwa na michezo  katika uwanja wa General Tyre katika  jiji la Arusha.

Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka linaandaliwa na Taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa Arusha(TASWA- Arusha chapter).

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa TASWA  mkoa Arusha, Mussa Juma, alisema tamasha hilo litashirikisha wanahabari  400 kutoka mikoa ya Arusha,Manyara, Kilimanjaro na Jijini Dar es Salam.

Juma alisema katika kongamano hilo mada mbali mbali zitatolewa na wabobezi katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na michezo na wanahabari watapata fursa kutambua zaidi mchango wa hayati baba wa Taifa katika michezo.

"Mwaka huu, tumeamua kuanza na kongamano ili kukumbushana wanahabari masuala mbali mbali ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu"alisema

Akizungumzia maandalizi ya Bonanza, mratibu wa bonanza hilo Andrea Ngobole  amesema katika tamasha hilo wanahabari na timu waalikwa watashiriki katika michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia, riadha, kukimbiza kuku .

"maandalizi yanakwenda vizuri lakini tunaomba wadhamini zaidi kujitokeza ili kufanikisha tamasha na Kongamano la wanahabari mwaka huu"alisema.

Alisema katika michezo timu ambazo tayari zimethibitisha kushiriki ni TASWA Dar es Salaam ambao ndio mabingwa watetezi, timu za Radio Sunrise,timu za vyuo vya Uandishi habari Arusha, Arusha one Radio, Triple A Radio, Radio 5, ORS Radio ya mkoa Manyara na TASWA Arusha.

"tutangaza zawadi hivi karibuni na pia wageni waalikwa kama ambavyo hufanyika kila mwaka"alisema.

No comments:

Post a Comment