MCHEZAJI wa
kimataifa, Simon Msuva leo ameonesha matunda yake ya kucheza soka ya kulipwa
katika timu ya Difaa Hassan El-Jadida ya
Morocco baada ya kuifungia Taifa Stars mabao dhidi ya Botswana.
Katika mechi hiyo ya
kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, Msuva
alikuwa mwiba mchungu kwa Botswana na mabao yake hayo yaliipa Stars ushindi wa
mabao 2-0.
Kwa matokeo hayo,
Stars imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kukwea kwenye viwango vya Fifa.
Msuva alianza
kupeleka shangwe kwa mashabiki wa soka nchini katika dakika ya sita, alipofunga
bao la kuongoza akiunganisha pasi ya Mzamiru Yassin kabla ya kuujaza mpira
wavuni.
Mchezaji huyo wa
zamani wa Yanga, Msuva aliiandikia Stars bao la pili katika dakika ya 62 baada
ya kuunganisha vyema pasi ya kichwa kutoka kwa Shiza Kichuya.
Katika mechi ya jana,
timu hizo zilishambuliana kwa zamu ambapo kuna wakati Botswana walikuja kasi na
nusura wapate bao mara kadhaa.
Hata hivyo, Stars
jana ilikuwa na nafasi ya kupata mabao zaidi, hasa dakika ya 59, mshambuliaji
wake Mbwana Samatta anayecheza soka ya kulipwa KRC Genk ya Ubelgiji nusura
apate bao, lakini akiwa na kipa wa Botswana, Mwampule Masule shuti lake lilidakwa.
No comments:
Post a Comment