4:27 – Kwa mara ya kwanza viongozi watakaoshinda leo wataapishwa mbele ya wapiga kura wao – Dr. Mwakyembe
4:22 – Mgeni rasmi, Dr. Harrison Mwakyembe amesimama kutoa nasaha zake kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapa leo
4:11 – Kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma, Mussa Chailu anazungumza sasa kutoa angalizo kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi
Mkutano mkuu wa TFF maalum kwa ajili ya uchaguzi mkuu umefunguliwa rasmi hapa St. Gasper mjini Dodoma. Wajumbe wamejitambulisha na taratibu zingine zinaendelea. Tutakuwa tunakuwekea hapa kila linalojiri katika mkutano huu.
Leo August 12, 2017 unafanywa uchaguzi mkuu wa TFF ili kuopata viongozi wapya watakaohudumu kwa kipindi cha miaka minne ijayo. Uchaguzi unafanyika mjini Dodoma ambapo wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF watapiga kura kuchagua viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa shirikisho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alipata fursa ya kuhutubia kwenye mkutano mkuu ambapo aliwaeleza wapiga kura aina ya viongozi ambao wanatarajiwa na watanzania wapenda soka kwa ajili ya kuongoza shirikisho la soka nchini.
“Viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usioteteleka kwa vishawishi vya mpito. Serikali inaamini tunawajumbe makini humu ndani wasioyumbishwa kwa kwa vishawishi vya muda, vishawishi vya mpito, wanaongozwa na dhamira njema na uzalendo wa hali ya juu ambao watatuibulia viongozi bora wa wa TFF wenye ari, moyo, uelewa, weledi ns uadilifu unaotakiwa wa kuipeleka soka yetu ngazi nyingine ya maendeleo.”
“Wajumbe 128 mtambue mmebeba dhamana kubwa ya mchezo wa mpira wa miguu nchini, watendeeni haki watanzania kwa kuwapa viongozi makini.”
“Kwa mara ya kwanza, viongozi tutakaowapata leo, tutawaapisha mbele ya wapiga kura wao. Tunataka tufuate kanuni na sheria kama zilivyo, kama huko ilikuwa inasahaulika leo tuta waapisha kiapo cha utii na uadilifu kuheshimu katiba yao wenyewe, wataapishwa na msajili ambaye ni wakili.”
“Umuhimu wa chaguzi wa leo kwetu sisi watanzania unajieleza wenyewe. Tuanataka uongozi utakaoilea iliyokuwa Serengeti Boys sasa ni Ngorongoro Heroes ili iiwakilishe nchi kwenye mashindano ya Olympic ya mwaka 2020 kwa wachezaji chini ya miaka 23.”
“Tunataka uongozi utakaoshirikiana na serikali kwa karibu kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mashindano ya AFCON kwa vijana wa umri chini ya miaka 17 yatakayo mwaka 2019 ambapo Tanzania tutakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.”
“Tunataka uongozi ambao utaanza mara moja kuinoa Serengeti Boys mpya inayotokana na vijana tuliowapata miaka miwili iliyopita kutokana na mashindano ya watoto chini ya miaka 13 ambao wanaendelea kunolewa na kuimarishwa kwenye academy moja hapa nchini, tunataka uongozi ambao utashirikiana kwa karibu na serikali kulea watoto wenye vipaji vya mpira wa miguu tuliowaibua kwenye mashindano ya hivi karibni mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA.”
“Uongozi unaotambua kwamba FIFA na CAF hawakumbatii rushwa na ubadhilifu kama ambavyo serikali hii haikumbatii rushwa wala ubadhilifu na uongozi ambao unajua kushirikiana na tutaupima uongozi huo katika miaka minne kwa hayo yote niliyoyataja.”
No comments:
Post a Comment