Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 12, 2017

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI AGAWA VIFAA VYA MICHEZO JIMBONI KWAKEMBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa  timu za jimbo hilo zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira  linaloshirikisha timu za wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na gazeti hili Ridhiwani alisema atawapatia  washindi wa pili wa michuano hiyo pikipiki ya miguu miwili na jezi kwa  timu zote tatu za juu na mshindi wa kwanza atapata zawadi ya bajaji toka kwa mkuu wa wilaya.
“Tumeamua kutoa zawadi ya pikipiki ili ziwasaidie vijana kuingiza kipato ili kuongeza ajira kwa vijana badala ya kuendelea kuwa tegemezi,” alisema Ridhiwani

Pia Ridhiwani alisema mashindano hayo yameandaliwa na Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge wa majimbo yote ya wilaya hiyo.
Hafla ya kugawa vifaa ilitanguliwa na mchezo wa soka kati ya timu ya Kata ya Kimange  na Mbwewe.