Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 18, 2017

VIINGILIO NGAO YA JAMII KULIPA KODI YA JENGO LA YANGA


UONGOZI wa Yanga umepanga kuweka utaratibu wa kulipa deni la sh 360 milioni kupitia mapato ya uwanjani ili kunusuru jengo la klabu hiyo lisipigwe mnada.
Gazeti moja la leo lilitoa tangazo la mnada wa majengo kadhaa kwa agizo la Mahakama  huku jengo hilo la klabu ya Yanga likiwemo baada ya kushindwa kulipiwa kulipiwa kodi tangu mwaka 1996.
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema kuwa wamepanga kuweka mikakati ya kulipa deni ambapo msimu ukianza watachukua sehemu ya mapato ya mlangoni na kutoka katika vyanzo vingine ili kulipa deni hilo.

“Ni kweli tunadaiwa deni hilo kutokana na kulimbikiza kodi ya majengo, tutaweka mpango wa kulipa kwa kuwasiliana na mamlaka husika na ligi ikianza tutachukua kiasi cha mapato ya mlangoni kupunguza deni,” alisema Mkwasa.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’  alisema pia uzembe umechangia kulifanya deni hilo kuwa kubwa ila uongozi utafanya kila liwezekanalo kulipa.