MPIGAPICHA
wa Tanzania Standard Newspapers Ltd na Mmiliki wa mtandao huu
Rahel Pallangyo amepata tunzo ya mpigapicha bora wa Mashindano ya Ndondo 2017 yaliyofanyika
kwenye Mkoa wa Dar es Salaam.
Mbali na
tunzo hiyo waandaji wa michuano hiyo walitoa tunzo mbalimbali kwa washindi, tunzo
binafsi, vikundi na tunzo za heshima.
Tunzo mwamuzi
bora ilichukuliwa na Nadim Mohamed, mwandishi bora alikuwa Charles Abel wa
Mwananchi, balozi wa Ndondo mchezaji wa Tottenham ya England Victor Wanyama,
shabiki bora alichaguliwa Jata Boy wa Misosi FC na Kitoto cha Ndondo.
Kwa upande
wa Wachezaji beki bora alikuwa Kashkash Kindamba wa Keko Furniture, kiungo
mshambuliaji bora ni Emanuel Pius kutoka timu ya Goms United, mfungaji bora ni
Rashid Roshwa wa Kibada One, mchezaji bora akaibuka Emanuel Memba wa Misosi FC.
Kipa bora ni
Haroun Mandanda wa Mlalakuwa Rangers, kocha bora ni Shabani Kazumba wa Goms
United, tunzo ya heshima ilitolewa kwa Juma Mwaka na Azam TV na kikundi bora
cha ushangiliaji ni Goms United.
Akizungumza
baada ya kukabidhi tunzo mgeni wa heshima, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani
Kikwete alipongeza waandaji wa mashindano hayo kwa kuibua njia mbadala ambayo
inawapa fursa wachezaji ambao hawana timu zinazocheza ligi inayotambulika.
“Niwapongeze
waandaji kwa kubuni njia mbadala ya kuwapa fursa vijana kuonesha vipaji vyao
hivyo naomba mamlaka za zinazosimamia soka kusaidia kuendeleza Ndondo,” alisema
Ridhiwani.
Pia Ridhiwani
alimpongeza Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia kwa
kuchaguliwa kuiongoza TFF na kusema ana imani na uongozi wake.
Hafla hiyo
ilihudhuriwa na Mjumbe wa Kamati ya utendaji TFF, Elias Mwanjala, mwenyekiti wa
Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo, Mwenyekiti wa Chama cha
soka Dodoma, Mulamu Nghambi, wadau mbalimbali wa soka, viongozi na baadhi ya
wachezaji wa timu zilizoshiriki mashindano hayo.
Tuzo ya heshima-Dr. Mwaka
No comments:
Post a Comment