Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 22, 2017

AZAM FC WAFANYA MABADILIKO YA UONGOZI




BODI ya Azam FC imemteua Mwanasheria Shani Christoms kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu, nafasi iliyooachwa wazi na Nassor Idrissa Mohammed 'Father'.
Awali, Shani alikuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu na katika mabadiliko haya, nafasi yake inachukuliwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’.
Akitangaza mabadiliko hayo mbele ya vyombo vya habari, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema aliyekuwa Mwenyekiti, Nassor Idrissa Mohamed ‘Father’ sasa anakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa bodi.
Idd alimalizia kwa kusema katika kuboresha safu ya uongozi wa timu hiyo, bodi hiyo imemteua Abdul Mohamed, kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC na kukifuta cheo chake cha awali cha Meneja Mkuu.
Wengine wanaounda sekretarieti hiyo ya Azam FC, ni Meneja wa timu, Phillip Alando na Ofisa Habari, Jaffar Idd.

No comments:

Post a Comment