Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, August 4, 2017

MAKUNDI YA LIGI DARAJA LA KWANZA YAPANGULIWABODI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya A na B katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyotarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Akizungumza na mtandao huu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniphace Wambura alisema timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi A sasa itakuwa kundi B wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa kundi B sasa itakuwakundi kundi A.
“Tumefanya mabadiliko kidogo katika kundi A na kundi B ili kuzipunguzia timu gharama za kusafiri umbali mrefu kucheza,” alisema Wambura
Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kundi yatakuwa kama ifuatavyo;,
Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashanti United, Friends Rangers, Mshikamano ya Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.
Kundi ‘B’  itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga, JKT Mlale ya Ruvuma, KMC ya Dar es Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufindi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na Mawenzi Market za Morogoro.
Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto Africans za Mwanza, Rhino Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Dodoma FC, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
Kila kundi litatoa timu moja itakayo kupanda daraja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19