KAMPUNI ya Vodacom Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi kuu imegawa vifaa vya michezo vyenye thamani ya
zaidi ya sh 500 milioni kwa timu zote 16 kuelekea kuanza kwa msimu mpya
wa ligi 2017/18.
Vifaa vilivyotolewa ni jezi, viatu vya mazoezi na mechi, soksi,
vizuia ugoko, nguo za mazoezi, mabegi ya kusafiria, jezi za waamuzi na
vibao vya kufanyia mabadiliko uwanjani ili timu hizo shiriki na bodi ya
ligi ziendelee na maandalizi kabla ya kuanza kwa ligi Agosti 26.
Mkurugenzi wa Idara ya masoko na usambazaji wa Vodacom, Hisham Hendi
amesema wamegawa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki kama mkataba
unavyoelekeza.
“Tunayo furaha kugawa vifaa vya michezo kwa timu shiriki
za ligi kwa mujibu wa mkataba tuliosaini, tuna imani ligi ya msimu huu
itakuwa ngumu kutokana na maandalizi yanayofanywa na timu zote,” alisema
Hendi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya ligi Boniface Wambura amezitaka
klabu kutumia nembo ya mdhamini mkuu kama ilivyoelekezwa ili kutokiuka
masharti na kuadhibiwa.
“Nataka nizikumbushe klabu kuhakikisha zinafuata makubaliano ya mkataba kwa kutumia vifaa vilivyotolewa,” alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment