WACHEZAJI wa
timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wanatarajiwa kugawana sh. Milioni 22
ambazo ni zawadi ya mshindi wa tatu kutoka katika mashindano ya Baraza la Mpira
wa Miguu kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa).
Akizungumza
na mtandao huu, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas
alisema COSAFA imetoa zawadi ya dola 10,000 sawa na Sh. 22,000,000 kwa Taifa
Stars baada ya kushinda na kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Castle
Cosafa yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.
“TFF imeamua
fedha hizo zitolewe kwa wachezaji wote walioshiriki fainali hizo pamoja na
benchi la ufundi pia Cosafa imetuma fedha za zawadi kwa wachezaji waliofanya
vizuri katika kila mchezo,” alisema Lucas.
Wachezaji hao
ni Shiza Kichuya aliyeibuka mchezaji bora wa mechi dhidi ya Malawi, Muzamiru
Yassin aliyeibuka mchezaji bora wa mechi dhidi ya Angola, Erasto Nyoni
aliyeibuka mchezaji bora dhidi ya Mauritius, Elius Maguri aliyeibuka mchezaji
bora wa mechi dhidi ya Afrika Kusini.
Pia Lucas
alisema kipa bora wa michuano hiyo ni Said Mohammed alizawadiwa moja kwa moja
na Cosafa.
Tanzania
ilishika nafasi ya tatu wakati Zimbabwe iliibuka bingwa na Zambia iliyshika
nafasi ya pili.
No comments:
Post a Comment