KAMPUNI ya New Habari (2006) LTD kupitia gazeti lake la DIMBA, imeandaa onesho maalum la muziki wa dansi DIMBA Music Concert litakaofanyika Septemba 2 mwaka huu katika Ukumbi wa Traventine Magomeni jijini Dar es Salaam.
Onesho hilo lina lengo la kuukuza na kupromoti muziki wa dansi ambao umekuwa ukielekea kupotea kila kukicha.
Katika
onesho hilo kutakuwepo na mpambano wa wanamuziki wa dansi, ambapo bendi
ya Msondo Ngoma Music (Baba wa Muziki), itachuana na mastaa mbalimbali
wa muziki huo kutoka bendi mbalimbali nchini.
Kundi la mastaa ambao wamepewa jina la ‘Timu ya Taifa ya Muziki wa Dansi,’ litakalochuana
na Msondo Ngoma, litaundwa na wanamuziki kama Kikumbi Mwanza Mpango
‘King Kiki’, Hassan Rehani Bitchuka ‘Stereo’, Karama Regesu, Ally Choki,
Juma Kakere, Nyoshi El-Saadat ‘Sauti ya Simba’ na Muumini Mwinjuma.
Kwa
upande wa vyombo, watakuwepo wapiga vyombo Saadi Ally ‘Machine’ kwenye
dramu, gitaa la solo litapigwa na Aldofu Mbinga wakati besi
litangurumishwa na Hosea Mhogachi.
Aidha,
kinanda kitapapaswa na Juma Jerry wakati tumba zikikung’utwa na Salum
Chakuku ‘Kuku Tumba’, ambapo ala za upepo watakuwepo Ally Yahaya, Hamis
Mnyupe Tarumbeta na Shaabani Lendi kwenye Saksafoni.
“Utakua
ni usiku wa mastaa wa dansi kuionyesha kazi Msondo Ngoma, kwani miaka
ya hivi karibuni imekua ikikosa mbabe katika kila bendi
inayoshindanishwa nayo lakini safari hii tumeamua tuwaonyeshe
kazi,”alisema meneja matukio wa Dimba Music Concert, Mwani Nyangassa.
Kiingilio
katika onesho hilo litakaloanza kuanzia saa 2:00 usiku hadi majogoo,
kitakuwa ni shilingi 10,000 kwa wote na 20,000/- kwa VIP.
No comments:
Post a Comment