KAIMU
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na Hamad Juma wamepitishwa kugombea
uenyekiti wa kamati ya Bodi ya Ligi Tanzania katika mchujo wa awali.
Akizungumza
na wadishi wa habari, Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
Alfred Lucas alisema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 15, Dar es
Salaam.
“Nafasi
zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watatu kuwakilisha klabu
za Ligi (PL), Wajumbe wawili wa kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza
(FDL), na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL),”
alisema Lucas.
Katika
nafasi ya makamu mwenyekiti ina mgombea mmoja ambaye ni Shani Christoms na kwenye
ujumbe wa timu za ligi kuu ni wawili pekee waliopitishwa wakati nafasi hiyo
inahitaji wagombea watatu.
Waliopitishwa
ni Hamis Madaki na Ramadhan Mahano na wajumbe wa timu za ligi daraja la pili
wwaliopitishwa ni Almas Kasongo na James Bwire na daraja la pili ni Edgar
Chibura.
Uchaguzi
huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
No comments:
Post a Comment