KOCHA Mkuu
wa timu za Vijana, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 50 wa timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20
‘Ngorongoro Heroes’ ambao wanatarajia kuingia kambini Oktoba Mosi.
Akizungumza Poulsen alisema timu hiyo inaundwa na wachezaji na wachezaji waliokuwa
Serengeti boys iliyoshiriki AFCON yaliyofanyika Gabon, mashindano ya timu za
U-20 na wengine wnatokana na mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA.
“Kuna wachezaji 23 wa
timu ya Serengeti Boys iliyoshiriki fainali za Gabon mwaka huu na walifanya
vizuri na sasa natarajia watafanya vizuri na kati ya hao 50 nitawachuja ili
kupata wachezaji 30 ambao wataunda kikosi cha Ngorongoro Heroes,” alisema
Poulsen.
Pia
Poulsen alisema wapo hata wachezaji hawakubahatika kwenda Gabon kutokana na
umri kuzidi na watafanya mazoezi pamoja kabla ya kuwachuja kupata wachezaji 30
ambao watakuwa wanaingia kambini kila mwezi.
Kambi
hii itakuwa ya wiki mbili ambapo wachezaji hao watakuwa chini ya kocha Kim
Poulsen, msaidizi wake Oscar Mirambo na kocha wa makipa Peter Manyika.
Awali
akizungumza Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas
alisema TFF imemteua Poulsen kuwa kocha mkuu wa timu za vijana za Serengeti
boys, Ngorongoro heroes na Kilimanjaro.
Awali
Poulsen katika uongozi wa TFF uliopita alikuwa mshauri wa ufundi wa timu hizo
na kocha alikuwa Bakari Shime kibarua ambacho kinaonekana kuota mbawa kwake kwa
sasa.
No comments:
Post a Comment