Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 12, 2013

TIMU ZA POLISI TANZANIA ZAAGWA, ZATAKIWA KUJILINDA NA UKIMWI PIA KURUDI NA USHINDI SARPPCO

Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye (kushoto) akimpa mkono nahodha wa timu ya Polisi, Makame Ally (kulia) wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wanaokwenda kwenye mashindano ya polisi kwa nchi zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara (SAPCCO) iliyofanyika Chuo cha Maafisa Polisi, Kilwa road leo.

Wanamichezo wa kiume wakimsikiliza mgeni rasmi

Wanamichezo waanawake wakimsikiliza mgani rasmi


Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye akizungumza  wakati akiwaaga wanamichezo



Wanamichezo wakiwa pamoja na maofisa wa polisi

WANAMICHEZO wa jeshi la Polisi Tanzania wanaokwenda kwenye michezo ya polisi kwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SARPPCO) wameagwa leo na Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye na kutahadharishwa kujilinda na ugongwa wa UKIMWI ili waweze kufanya vizuri kwenye michezo hiyo.

Akizungumza kabla ya kukabidhi bendera Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye alisema lengo la michezo hiyo ni kuwafanya wafahamiane na polisi wa nchi zingine pia kubadilishana mbinu za kupambana na uhalifu.

Timu zinazokwenda kwenye mashindano hayo ni soka, mpira wa pete (netboli) darts na riadha ambapo wanamichezo 67 ndio waliokwenda.

No comments:

Post a Comment