WACHEZAJI
wapya wa Simba, Emmanuel Okwi na Niyonzima
wamewapagaisha mashabiki wakati timu hiyo ikiibuka na ushindi wa bao 1-0
dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.
Mchezo huo
uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ulikuwa maalumu kwa
ajili ya kuadhimisha Simba Day, ambayo kilele chake kilikuwa leo.
Bao hilo
pekee lililonogesha pilau la Simba, liliwekwa kimiani na Mohammed Ibrahim
katika dakika ya 16 kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na John Bocco 'Adebayoy'.
Mashabiki
walilipuka kwa shangwe pale Okwi na Haruna Niyonzima walipotambulishwa rasmi
mbele ya mashabiki wa timu hiyo uwanjani hapo.
Mbali na
kuwatambulisha wachezaji wao wapya, Simba pia ilitoa tuzo kwa mchezaji wake wa
zamani, Abadallah Kibadeni kwa kuisaidia timu hiyo kuifunga Yanga kwa mabao 6-0
baada ya kufunga bao tatu peke yake (hat-trick) mwaka 1977.
Pia Kibadeni
alipewa tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu hiyo kucheza fainali ya Kombe la CAF
mwaka 1993.
Mohammed
Hussein `Tshabalala’ amepewa tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita
aliyechaguliwa na mashabiki wa timu hiyo.
Simba
iliuanza mchezo huo kwa nguvu, ambapo Okwi nusura afunge katika dakika ya 11,
lakini kipa wa Rayon aliupangua mpira.
Simba kila
mwaka imekuwa ikiandaa tamasha la Simba Day, ambalo wamekuwa wakilitumia
kuwatambulisha wachezaji wao wapya na jezi zao mpya zitakazotumika msimu ujayo
nyumbani na ugenini.
Kikosi cha
Simba;
Aishi
Manula, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, Method Mwanjali, Salum Mbonde/Yussuf
Mlipili, James Kotei/Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Said Ndemla, Muzamir Yasin,
Mohamed Ibrahim/Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi/Nicolaus Gyan na John Bocco `Adebayor’/Laudit Mavugo.
No comments:
Post a Comment