OFISI za
Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam zimevamiwa na watu sita wanaodhaniwa
majambazi na kupora komputa mpakato, simu mbili na fedha zaidi ya sh. milioni
mbili.
Ofisi hizo
zipo ghorofa ya tatu katika jengo la Machinga Complex Ilala.
Akizungumza
na wandishi wa habari leo, Katibu wa Chama cha Soka Ilala (IDFA) Daud Kanuti
ambaye ni mmoja wa watu walioporwa mali zao alisema tukio hilo lililokea majira
ya saa nne asubuhi.
“Nilifika
ofisini majira ya saa nne nikamkuta mtu amekaa mapokezi huku akiwa ameshika
radio ya upepo (radio call) na pingu baada ya kuingia ndani akaniamrisha nimpe
ufunguo wa ofisini kwangu,”
“Baada ya
kumpa akanifunga pingu huku akinisukuma kupandisha kwenye vyumba vya ofisi
zilivyo ghorofani nilipofika huko nikakuwakuta wenzangu wakiwa wamefungwa kamba
miguuni na mikononi na mimi wakanifunga pia,” alisema Kanuti
Kanuti
alisema watu hao ambao hawakuficha sura zao walikuwa wakimwambia awape fedha
ambazo zipo ndani ya ofisi na walimwambia ni sh. milioni 150.
Pia Kanuti
aliwataja wenzake ambao walikuwepo ofisini kuwa ni Ofisa Utawala wa DRFA, Said
Pambalelo, wahudumu wawili wa ofisi Ally Rashid na Ramadhan Kondo na Faisal
Siri nahodha wa Nungu FC ambaye alikuja kuchukua fomu za usajili.
Aidha
alisema pesa zilizochukuliwa ni zaidi ya sh. 1,200,000 ambapo sh 450,000 ni
fedha za za usajili wa klabu zilikuwa ndani ya ofisi na nyingine zimeporwa
kwenye mifuko yao.
Thamani
zingine zilizochukuliwa ni komputa mpakato mali ya Pambalelo na simu ndogo
mbili.
Muda mfupi
baada ya tukio hilo kutokea askari wa kituo cha Polisi Pangani na Msimbazi
vyote vya Ilala walifika na kuchukua maelezo ya awali na baadae waliondoka nao
hadi kituo cha polisi Msimbazi kwa maelezo zaidi.
No comments:
Post a Comment