Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 3, 2017

SIMBA KUISHTAKI KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI CAS



 
UONGOZI wa Simba umesema unasubiri kupewa barua na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inayoonyesha kweli wamepokwa pointi tatu za mchezo dhidi ya Kagera Sugar ili wakashitaki katika Mahakama ya usuluhishi ya FIFA (CAS) .
Simba ambayo ilipoteza mchezo huo mabao 2-1, ilikabidhiwa pointi tatu baada kamati ya usimamizi na uendeshwaji wa ligi (Kamati ya saa 72) kujiridhisha kuwa Kagera walimchezesha beki Mohamed Fakih ambaye alikuwa na kadi tatu za njano kabla ya mchezo huo pointi ambazo baadae zilirejeshwa kwa Kagera na kamati ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Rais wa klabu hiyo Evans Aveva amesema hawawezi kukubali kuona timu yao inaonewa tena na TFF na kwa kuanzia wanasubiri wapewe barua ya kuporwa pointi tatu hizo ili wapeleke malalamiko yao CAS.
“Tumeonewa mara nyingi, mfano suala la wachezaji Mbaraka Yusuph, Hassan Kessy na Ramadhan Singano ‘Messi’ walikuwa wachezaji wetu halali lakini TFF wakawaidhinisha kucheza timu nyingine, huu ni uonevu tumechoka kuonewa tunaenda FIFA,” alisema Aveva.
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 59 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56 na michezo miwili mkononi ambayo ikishinda yote itaizidi Simba kwa pointi tatu.

No comments:

Post a Comment