Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 3, 2017

AVEVA ASHANGAA HAHI MANARA KUHUKUMIWA BILA KUSIKILIZWA



RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) haikutenda haki kumfungia msemaji wa timu hiyo Haji Manara bila kumpa nafasi ya kumsikiliza kutokana na kupata dharura.
Aprili 23 kamati hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti  Wakili Jerome Msemwa ilimfungia Manara mwaka mmoja na faini ya Shilingi milioni tisa kwa kosa la kutamka maneno yasiyo na staha kwa viongozi wa Shirikisho hilo.
Aveva alisema hayo mbele ya wandishi wa habari kuwa hakukuwa na haraka kutoa hukumu hiyo bila ya kumsikiliza msemaji huyo kwakuwa klabu ilipeleka barua TFF kuomba hukumu isogezwe mbele kwani Manara alikuwa nje ya mji akishughulikia mambo yake.
“Hili suala kama uongozi wa Simba limetushangaza sana. Hatukuona sababu ya Kamati ya nidhamu kuwa na haraka wa kiasi hicho kutoa hukumu bila kumsikiliza mshitakiwa ambaye klabu ilikuwa imemtolea udhuru.
“Kuna mambo mengi yanachelewa kutolewa maamuzi lakini suala la Manara aliyekuwa akiitetea klabu limeamuliwa haraka bila hata kumsikiliza mshitakiwa,” alisema Aveva.
Pia Aveva alisema wamesikia fainali ya michuano ya kombe la FA itanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo kwa upande wao wamesema kwa ukubwa wa mshindano hayo yalipaswa kufanyikia Uwanja wa Taifa ila hawana kipingamizi na maamuzi ya TFF.

No comments:

Post a Comment