Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 5, 2017

KOCHA WA KUOGELEA KUFANYA ZIARA NCHINI



UJIO wa Kocha Sue Purchase kutoka katika shule ya kimataifa ya Mtakatifu Felix Uingereza kusaka vipaji vya mchezo wa kuogelea kwenye mashindano ya taifa kutawanufaisha wachezaji watakaoonyesha uwezo.
Mashindano ya klabu bingwa Taifa yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii na kushirikisha wachezaji 172 kutoka klabu 15 za Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka, Purchase ambaye pia  ni Mkurugenzi wa michezo wa kuogelea wa shule hiyo, lengo ni kusaka vipaji vya mchezo huo.
“Wachezaji Sonia Tumiotto, Collins Saliboko, Anjani Taylor,  Smriti Gokarn na Aliasgar Karimjee ambao wanasoma Uingereza tayari wameshawasili nchini kushiriki mashindano ya Taifa na wanaendelea na mazoezi ya Dar es Salaam,” alisema.

Namkoveka alisema kuwa waogeleaji wameonyesha viwango vya hali ya juu kiasi cha kumfanya Purchase kuamua kuja nchini kushuhudia waogeleaji wengine wa Tanzania  katika mashindano hayo
Alisema kuwa mbali ya kushuhudia mashindano hayo na kusaka vipaji, kocha huyo atakutana na wazazi, makocha, waogeleaji wa klabu ya Dar Swim Club na kufanya  nao mazungumzo.
Alisema kuwa hii ni faraja kwa wadau, wachezaji, Klabu  na viongozi wa mchezo wa kuogelea kwani ujio wa kocha ni ishara ya mchezo kukua.
Mashindano hayo yatashirikisha klabu 15 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambazo zitashindana katika staili za backstroke, freestyle, breaststrokes, Butterfly na Individual Medley (IM).

No comments:

Post a Comment