Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, April 6, 2017

TANZANIA YAPANDA NAFASI 22 KWENYE VIWANGO VYA UBORA FIFA

TANZANIA imepanda kwa nafasi 22 kwenye viwango vya ubora wa soka kwa wanaume Machi kufuatia matokeo mazuri iliyoyapata katika michezo ya kirafiki ya kimataifa hivi karibuni.
Februari mwaka huu Tanzania ilikuwa nafasi ya 157 huku katika viwango vilivyotangazwa leo na FIFA ikikamata nafasi ya 135.
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliifunga Botswana mabao 2-0 kabla haijaibutua Burundi 2-1 mwishoni mwa mwezi uliopita.
Brazil imeipiku Argentina katika nafasi ya kwanza huku Ujerumani ikishika nafasi ya tatu.