Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 5, 2017

BASI LA TFF LAACHIWA, TRA YAOMBA RADHI WATANZANIA




MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka mashabiki wa soka nchini kutambua kuwa inalijadili kwa kina tukio la kukamatwa kwa basi lililokuwa limebeba wachezaji wa timu ya Serengeti juzi.
Juzi basi lililokuwa limebeba wachezaji wa timu hiyo majira ya jioni katika eneo la Kisutu lilikamatwa na kampuni ya Udalali ya TRA, Yono Auction Mart wakati likiwapeleka wachezaji hao kwa Makamu wa Rais kwa ajili ya chakula cha usiku.
Msemaji wa TRA, Richard Kayombo alisema kuwa Mamlaka hiyo imesikitishwa na kitendo hicho na kuwa inaendelea na mazungumzo ya ndani kuona ni hatua gani ya kuchukua.
Alisema, TRA ni sehemu ya wananchi na timu hiyo ni timu ya wananchi ambapo imekuwa ikijiandaa kuiwakilisha nchi kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17.
Aliongeza kwa namna yoyote ile wachezaji hao hawakutakiwa kubugudhiwa kiakili na kwa kitendo cha kushushwa kwenye basi kwa kuwa ni Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ndio linalodaiwa.
“Tunapenda kuwaomba radhi na pia kulaani kwa kitendo kile kwa kuwa kwanza sio uungwana na pili ilitakiwa kutumika kwa hekima zaidi na sio kile kilichofanyika pale, kwa kweli TRA inalifuatilia kiundani suala hilo kwa sasa” alisema Kayombo.
Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa Yono Auction Mart, Stanley Yono alisema kuwa kampuni yake ilikuwa ikitekeleza maagizo ya serikali ya kukusanya wadaiwa wa TRA.
“Kwa sasa ninachoweza kusema ni kuwa maafisa wa kampuni hii walikuwa kwenye utekelezaji wa majukumu yao na hiyo ilikuwa ni sehemu ya kazi hiyo” alisema Yono.
Timu hiyo imeondoka jana mchana kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya kujiandaa na Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana itakayofanyika nchini Gabon mwezi Ujao.
TRA imezifungia ofisi za TFF kwa kile kinachodaiwa kuwa ni malimbikizo ya kodi za mishahara ya aliekuwa kocha wa Timu ya Taifa, Marcio Maximo kwa miaka minne tangia mwaka 2006 hadi 2010.
Pia kuna sakata na Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) linalotokana na ziara ya timu ya Taifa ya Brazil nchini mwaka 2010 ilipokuwa njia kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment