Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, April 5, 2017

MAKAMU WA RAIS AIPA NENO SERENGERI BOYS KABLA YA KUPAA KWENDA GABON
MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu amewataka wachezaji wa timu ya soka ya Taifa ya Vijana U-17 ‘Serengeti Boys’ kujitahidi kupata ushindi ndani ya dakika 90 na siyo kutafuta ushindi wa kulazimisha dakika za lala salama.
 Hayo aliyasema juzi, wakati wa chakula cha usiku alichowandalia wachezaji hao kuwaaga kabla ya jana kusafiri kwenda Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mashindano ya vijana ya Afrika (AFCON, U-17)
 “Matokeo ya mechi dhidi ya Ghana yalikuwa mazuri lakini yalinipa hofu kidogo kwa sababu kilichotokea ilikuwa ni miujiza kwani ndani ya dakika 10 mlirudisha mabao mawili, sio kitu rahisi, kwa kawaida maajabu huwa yahana kanuni, kwa hiyo naomba msicheze kwa maajabu, chezeni ndani ya dakika 90,” alisema Mama Samia alipokuwa na Serengeti Boys nyumbani kwake.
Pia Samia alisema kilichotokea kwenye mchezo huo akiwauliza walitumia formula gani hawawezi kueleza ni uwezo wa Mungu kutaka yale yatokee na kuomba wasicheze hivyo wahakikisheni dakika 90 zinakwisha wakiwa na ushindi
Aidha mama Samia alisema isingekuwa Ghana kujiangusha na Serengeti boys kupata dakika nyingi za nyongeza wangefungwa kujiangusha ndio kulizaa dakika 10 wakaweza kupata sare
Pia alitoa wito kwa viongozi na benchi la ufundi kuishi na kuwalea wachezaji hao kama marafiki lakini kuwarekebisha kwa kuwachapa pale wanapokosea na utukutu unapozidi kwani huruma hailei mwana.
 “Vijana wanahitaji matunzo mema, hamasa, upendo, mshikamano na kupendana wao kwa wao kupendwa na walimu na viongozi ndivyo wanaweza kufanya vizuri hivyo tunawakabidhi hii timu, mnakwenda nje ya nchi mtakaa kwa muda mrefu, hatupendi kusikia lolote baya limetokea kwa hawa vijana,” alisema Samia.
Wakati timu hiyo ikiwa njiani kwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais, wachezaji pamoja na viongozi walishushwa kwenye basi na kampuni ya udalali ya Yono ambao ni wakala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitendo ambacho kimsikitisha Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe alisema ni aibu kwa taifa katika kipindi hiki ambacho kuna kampeni za kuhamasisha watanzania na wachezaji ili timu ifanye vizuri na watu wengine wanarudisha nyuma jitihada zinazofanywa.
“Vijana wetu walikuwa wanakuja kwako basi lao likasimamishwa na watu wa TRA wakaondolewa kwenye basi likachukuliwa, ikabidi viongozi wa TFF waanze kutafuta gari lingine, sijui wameingia kwenye daladala ndiyo wamewaleta hapa,” alisema Mwakyembe
Pia Dk. Mwakyembe alisema suala la kodi ni suala muhimu na ni lazima kila mtu alipe kwani halina msamaha, lakini akawasisitiza TRA kutumia busara katika kukusanya kodi.
“Namwagiza katibu wangu mkuu kukaa na katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na viongozi wa TRA pamoja kwani haya mambo yanatia aibu timu inakwenda kwa kiongozi wa nchi, wewe ndio unaona fursa kwako, nani atakupa mamilioni ya fedha kwa kusimamisha magari barabarani?” alihoji Dk. Mwakyembe.
Pia Dk. Mwakyembe wanawatengenezea biashara Yono kwa sababu mwaka jana alisoma kwenye magazeti walichukua gari la TFF, waliporudisha ikabidi TFF ilipe Yono milioni 20 kwa kushika lile gari na kusema ataiagiza TAKUKURU wafuatilie hiyo fedha isiende Yono.
 Aidha Dk. Mwakyembe alimwambia Mama Samia ikishindikana atakwenda kushitaki kwake kwani hataki kusikia tena hilo deni kwa sababu ni aibu kusema mbele za watu kwa sababu ni wao wenyewe ndani ya serikali waliojichanganya.
Baadae jana Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema amekabidhiwa basi hilo na kampuni ya udalali ya Yono ambayo ni wakala wa TRA na kusema uongozi wa TRA umesikitishwa na kitendo hicho kisichofuata utaratibu na kuwashusha wachezaji.
Serengeti boys imeondoka jana saa 10:45 na Ndege ya Emirates kwenda Morocco kupitia Dubai , Falme za Kiarabu  (UAE)  na wachezaji 23 na viongozi nane