MABINGWA wa
soka Tanzania Bara, Yanga leo wameachana rasmi na Mkurugenzi wao wa Ufundi,
Mholanzi Hans van Der Pluijm.
Kwa mujibu
wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali na kuthibitishwa na kocha huyo wa zamani wa
Yanga, vinasema kuwa, timu hiyo imeachana rasmi naye.
Akithibitisha
hilo Pluijm alisema Yanga wamemuandikia barua ya kukatisha mkataba wake
kutokana na klabu hiyo kukumbwa na matatizo ya fedha.
"Ni kweli Yanga wamenipa barua ya kukatisha mkataba wangu na
sababu kubwa ni kutokana na matatizo ya fedha yanayowakabili kwa sasa, “alisema
Pluijm kwa kifupi.
Awali,
Mholanzi huyo alitua Yanga kama Kocha Mkuu na baadae kuachana na timu hiyo
kabla ya kurejea tena na kuwa kuendelea na nafasi yake.
Hata hivyo,
Pluijm alikatisha mkataba wake baada ya Yanga kumchukua kocha wa Zesco ya
Zambia, George Lwandamina kuchukua nafasi yake bila ya kumtaarifu.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Mchemba alimshawishi Pluijm kurejea Yanga,
lakini sasa akiwa Mkurugenzi wa Ufundi badala ya Kocha Mkuu.
Alisema kwa
sasa hawezi kulizungumzia suala hilo, kwani yuko katika harakati za maandalizi
ya mchezo wao dhidi ya Mtibwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Alisema timu
yao itaondoka kesho asubuhi kwenda Morogoro na jioni itafanya mazoezi kwenye
uwanja huo uliofanyiwa ukarabati hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment