Friday, March 3, 2017
DALALI AWANG'ATA SIKIO VIONGOZI SIMBA
MWENYEKITI wa zamani wa timu ya Simba Mzee Hassan Dalali ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumalizana na wanachama 72 waliopeleka kesi mahakamani ili kuendeleza umoja na kuondoa makundi ili kupata ubingwa msimu huu.
Dalali alisema kwa sasa umoja umeanza kurejea ndani ya klabu hiyo ambapo amekiri kama utaendelea hadi mwisho wa msimu kuna uwezekano mkubwa wa Simba kuibuka na taji la ligi kuu msimu huu.
Mwenyekiti huyo alisema umoja ulioonyeshwa kwenye mchezo uliopita dhidi ya watani wao Yanga na kuibuka na ushindi kama ukiendelezwa na kumaliza tofauti na wanachama hao basi kila kitu kitakuwa sawa.
“Namuomba Rais Aveva amalizane na wanachama hao ili umoja uliopo ndani ya klabu uendelee kuimarika kuhakikisha ubingwa unapatikana msimu huu” alisema Dalali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa Ustadhi Masoud ametangaza siku ya Jumapili Machi 4 watafanya usaili wa kuhakiki wanachama wa tawi hilo ili kuwapunguza na kubaki 250 kwa mujibu wa katiba ya klabu ya Simba.
Tawi la mpira pesa kwa sasa lina wanachama zaidi ya 750 ambao ni kinyume na katiba ya klabu hiyo ambayo inataka wanachama katika kila tawi wasizidi 250.
“Tutaanza kufanya usahili wa kuhakiki wanachama Jumapili utakaoendelea kwa siku sita ili kuendana na taratibu za klabu yetu ambayo inataka wanachama katika kila tawi wasiwe zaidi ya 250” alisema Ustadh.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment