Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, March 14, 2017

SERENGETI BOYS KAMBINI TAYARI KWENDA GABONTIMU ya Taifa ya soka ya vijana wenye umri wa miaka 17 'Serengeti Boys' imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala,  Dar es Salaam kujiandaa na Fainali za Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14.
Awali fainali za Afrika zilikuwa zianze Mei 21 lakini zimerudishwa nyuma hivyo Serengeti Boys itakuwa kambini, Dar es Salaam hadi Machi 26 itasafiri kwenda Kagera kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za vijana za Rwanda, Burundi na Uganda.
Michezo hiyo ambayo itachezwa katika Uwanja wa Kaitaba Serengeti boys itacheza na  Rwanda Machi 28, Burundi Machi 30 na Uganda wataumana nao Aprili 2.
Baada ya mechi hizo watarejea tena Dar es Salaam Aprili 3, ambako itaagwa na kukabidhiwa bendera ya Taifa na Aprili 5 itasafiri kwenda Morocco kwa ajili ya kambi.
Ikiwa Morocco kwenye mji wa Rabat itacheza michezo ya kimataifa ya kirafiki na Cameroon na Misri na Mei 6 itakwenda Gabon tayari kwa mashindano kwani wanatakiwa wawe wamewasili Mei 7.
Serengeti Boys imepangwa kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola ambapo fainali hizo zinajuisha mataifa nane ya Afrika, endapo Serengeti itafuzu nusu fainali itakuwa imekata tiketi ya kucheza fainali za dunia za vijana zitakazofanyika India, Novemba.