Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, March 14, 2017

HASSAN KABUNDA MCHEZAJI BORA WA FEBRUAI LIGI KUUMCHEZAJI wa Mwadui FC, Hassan Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wa Februari kwa msimu wa 2016/2017.
Akizungumza na gazeti hili, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema Kabunda aliwashinda wachezaji Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib wote wa Simba.
"Katika mechi tatu ambazo Mwadui ilicheza Februari Kabunda alicheza kwa dakika zote 270 na kuisaidia timu yake kukusanya pointi sita zilizoifanya ipande kwa nafasi mbili katika msimamo wa ligi," alisema Lucas.
Pia Lucas alisema Kabunda alifunga mabao manne katika mechi hizo tatu kati ya sita iliyofunga timu yake na kuisaidia Mwadui kupanda kutoka nafasi ya nane hadi ya sita.
Kiungo huyo mshambuliaji alionesha nidhamu ya hali ya juu kwani hakupata onyo lolote la mdomo au kadi kutoka kwa waamuzi.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Kabunda atazawadiwa kitita cha Shilingi 1,000,000 kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo.