Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 8, 2017

SIMU YAMPONZA WEMA KUENDELEA KUSOTA RUMANDEWAKATI wenzake wakipandishwa kizimbani juzi wakituhumiwa na kesi za dawa za kulevya,  Wema Sepetu ameendelea kusota rumande kwa matumizi ya simu ya mkononi huku akiwa ameshikiliwa na jeshi la Polisi.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kudai ni makosa katika nchi hii ukiwa yupo chini ya ulinzi halafu kuendelea kutumia simu ya mkononi.
“Matumizi ya simu watu wakiwa gerezani yamekuwa yakitumika kuendeleza biashara za dawa za kulevya kwa njia ya mawasiliano hata kama wakiwa ndani,” alisema Makonda.
Makonda alisema  amezungumza na wakuu wa Magereza yote yaliyopo Dar es Salaam na wakuu wa mikoa juu ya vitendo vya watu kuingia na simu katika vituo vya polisi.
Wema alikuwa akituma Video na sauti mbalimbali kuhusu hali ya maisha akiwa mahabusu ya kituo cha kati huku akimkejeli mkuu wa mkoa hivyo huenda akaendelea kuwa katika wakati mgumu kutokana na kitendo hicho cha kutumia simu akiwa mahabusu.